Jumapili 1 Novemba 2026 - 07:06
Usitosheke na Kumtegemea Mwenyezi Mungu tu Katika Jambo Lako, Bali ni Lazima na Wewe Ujibidiishe

Hawza/ Imamu Ridhaa (as), katika riwaya, anaashiria uhusiano uliopo baina ya kumtegemea Mwenyezi Mungu na kufanya juhudi katika maisha.

Shirika la Habari la Hawza, limechapisha riwaya ifuatayo kutoka katika kitabu cha Kanzul- Fawa'id.

Imamu Ridhaa (as) amesema:

«مَنْ سَأَلَ اللّهَ التَّوْفِیقَ وَلَمْ یَجْتَهِدْ فَقَدِ اسْتَهْزَأَ بِنَفْسِهِ.»

“Yeyote anayemuomba Mwenyezi Mungu amjaalie tawfiki, lakini asifanye juhudi, kwa hakika amejidhihaki mwenyewe.”

Rejea: Kanzu Al-fawa'id, Juz 1, Uk 330.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha